Magazine Sauti ya pwani 246 Final
Transcrição
Magazine Sauti ya pwani 246 Final
Vijana wajitokeza kujiunga na huduma za vijana picha zaidi uk. Wa 11 MASHAMBULIZI Vurumai za Tana Delta soma uk. Wa 4 auti ya S Pwani Kichocheo Kwa Turathi Za Pwani SAUTI YA PWANI Novemba 2012 Kandanda ya viziwi yazindua msisimko mpya Na Paul Olale- Kaunti ya Kilifi imu ya soka ya viziwi ya Malindi iliichabanga timu ya viziwi ya Makupa PCEA, Mombasa, 3-0, katika mchuano wa kirafiki katika uga wa kijamii, mjini Mombasa. Nyota ya mechi, Antony Kadenge, ndiye aliyejaza wavuni mabao hayo yote matatu, Katika kipindi cha pili Kadenge alilifunga bao la pili dakika ya 47, na la tatu dakika ya 64. Mechi hiyo iliwavutia mashabiki wengi mno, waliokuja tu kuthibitisha kama kweli viziwi wengeweza kusakata soka barabara. Mechi hiyo ilikuwa mojawapo ya misururu ya michezo ya viziwi yanayoendelea eneo la pwani , na yaliyotayarishwa na ushirika wa viziwi nchini, tawi la Malindi. Mtayarishi wa michezo hizo tawi la Malindi, Bi Priscilla Kibicho, alisema madhumuni yake ni kuihamasisha umma kutambua uwezo na haki ya wale wenye ulemavu mbalimbali,ili kwamba kusaidia kuondoa ubaguzi na unyanyapaa. Bi. Kibicho ana ulemavu wa kusikia, na ni mwalimu walugha ya ishara ya viziwi, mjini Malindi. KALOLENI WEMA BUTCHERY Dondokwa na mate!!! Nyama Bora Iwe ni ya choma, chemsha au karanga auti ya S UTAIPENDA Nambari zetu za simu 0728786868 0739820182 Pwani Kichocheo Kwa Turathi Za Pwani TOLEO NAMBARI 246 NOVEMBA 2012 BEI 30.00 YALIYOMO ? Viongozi wataka amani k. 10 ? Athari za ukame zazua maafak. 4 ? Kondoo mweusi atimuliwa kanisani uk. 12 T Ahitaji msaada kugharamia uuguzi Si vita… la hasha! Mchezo wa karate umenoga katika Kaunti ya Kilifi, wakubwa kwa wadogo Mashtuko baada ya mashambulizi ya Tana Delta Ahitaji msaada Vijana wakipokea tuzo na shani baada ya kushiriki kwenye mchezo wa karate uliofanyika huko Kilifi hivi majuzi Kutoka uk. Wa 8 na uharibifu wa viungo kuonekana hivyo basi kuzusha kero baina ya jamii na ukosefu wa fedha wakati wa kutaka matibabu. Shirika la WHO linapendekeza kuwa maeneo yote yaliyoathiriwa yatambuliwe ili miradi ya matibabu ianzishwe na kutibu watu wote wanaotishiwa na kuambukizwa kwa matende kwa muda usiopungua miaka mitano. Njia nyingine ni kuwawinda na kuwazuia mbu kusambaza viini kwa kutumia neti zilizotibiwa. Ingawa Abdalla hana ufahamu kuhusu miradi ya serikali kuhusu tiba za matende, ana matumaini kuwa siku moja atapata wafadhili ili naye aweze kuishi maisha ya kawaida tena. Iwapo umeguswa na hali hii ya Abdalla na ungependa kutoa msaada wa hali na mali unaweza kuwasiliana naye kwa rununu 0724257376 au 07752551906 ama uwasiliane na Abdalla Mwangade, Post Bank-Ukunda Branch A/c 0428010090974. Gazeti Hili Huchapishwa na Wizara ya Habari na Mawasiliano S.L.P. 421-Mariakani e-mail: [email protected] Na Nyambura Ngugi na Abdullahi Hussein, Kaunti ya Mombasa Yusuf Abdalla ni mzaliwa na mwenyeji wa Pwani ambaye amekuwa akiugua ugonjwa wa matende kwa zaidi ya miaka 13 sasa. Madaktari wamemtangazia kuwa mguu wake wa kushoto hauna manufaa kwake tena kutokana na athari za ugonjwa huo na njia iliyobakia ni kuukata. Haya ndiyo masaibu yanayomkumba na anahitaji kwa dharura msaada wa kimatibabu na fedha ili atimiziwe matibabu ya kukatwa mguu. Kulingana na wauguzi matende husababishwa na aina ya minyoo ambayo hufurisha miguu na mikono na hata sehemu nyeti za wanaume. Inaendelea uk. Wa 8 Wafanya Ngono Hadharani Taarifa ya Rajab Ramson Mzee na kuandikwa na Paul Olale Kaunti ya Kilifi W anaume wawili waimbaji nyimbo za kitamaduni ya Kigiriama (msego), waliafikiana kwamba iwapo mmoja wao atakufa basi atakaye bakia afanye mapenzi na mke wa mweziwe juu ya kaburi baada ya mazishi, la sivyo atakayekaidi afe pia. Kwa hivyo hivi majuzi siku hiyo ilitimia baada ya mwimbaji aliyetoa wazo hilo kuaga dunia akiwa na umri wa miaka 48,kijiji cha Mpirani, kata ya Gongoni, wilaya ya Magarini.Kakaze marehemu walisisitiza ahadi hiyo lazima itimizwe. Kwa hivyo ilivyo kawaida ya matanga katika maeneo haya, pombe ya mnazi uliletwa, na watu kubugia kwa fujo. Marehemu alizikwa saa nane mchana, nakuwekwa kando kando ya kaburi.Mzee mmoja kisha aliwaamuru wanawake kuchangia leso zao, ambazo zilitundikwa kwa vijiti vile na kuuzingira kaburi. Basi mjane wa marehemu, miaka 36, na yule mwimbaji walisukumwa ndani ya pazia zile, na kuagizwa kufanya mambo. Baada ya dakika kumi vishindo za mateke kwenye zile leso ziliashiria kwamba kazi ilikuwa ikiendelea, na watu wakaanza kupiga makofi na kuwamiminia sifa wawili hao, kwa majina ya matani. Dakika kumi zaidi, kwa sababu walikuwa juu ya mchanga wa kaburi usio thabiti, waliteremka hadi ukingo wa pazia, na miguu yao yakaanza kujipenyeza katika mianya ya leso. Baadhi ya wazee walihofia kuanguka kwa ua wa leso na kuwaacha uchi, na wakamfokea jamaa yule kutozidisha mpira, kwani uwanja ulikuwa mdogo. Mechi hiyo ya ajabu ilichukua nusu saa, na kisha mume alijitokeza kwenye uwanja wa kaburi amelowa jasho kama aliyeoga, huku akichechemaa kwa uchovu. Mke naye alibakia kule ndani, hadi wanawake watatu wakongwe walipongia pale na kumnyanyua na kumpeleka kumlaza chumbani. BUTWAA NA AIBU Haikujulikana mara moja kilichomtendekea; pengine uchovu, kupigwa na butwaa, aibu, ulevi au mchanganyiko wa vyote. Baada ya hapo shughuli ya matanga ziliendelea kwa siku tatu, na waliosisimuliwa na tukio hilo wakachangia’ombe watatu na mbuzi waanne wakachinjwa, na mitungi 20 ya mnazi kumiminwa. Kisa hicho kimebakia kama ngano katika ndimi za watu wa sehemu hiyo, kwani ni cha kwanza kutendeka. Gazeti hili hufikia kaunti za: Mombasa, Kwale, Kilifi, Lamu, Tana River na Taita Taveta TAITA FEEDS MANUFACTURES OF: MINISTRY OF INFORMATION AND COMMUNICATIONS GROWERS, LAYERS, CHICK AND BROILER MASH & SUPER DAIRY MEAL LOCATED AT MCHARO’S BULIDING, SHIGHARO ROAD. DEPARTMENT OF FILM SERVICES OFF WUNDANYI BUS TERMINUS ADVERTISEMENT P.O. BOX 1128 WUNDANYI CELL: 0722 796 783/0738 402 231/0722 971 622 Email: [email protected] For affordable prices and door step delivery of all livestock feeds. Targeted people include, Commercial Photographers, Video/Studio operators/ Film Makers both local and International. Please note that it is now mandatory under cap 222 of Film and stage plays act to first obtain a film license before engaging in any film production or practice. Please visit the department of film services offices located at SAUTI House, First floor, Mombasa City or any Information office near your area for more information. You can be licensed as an Individual or as a Group 14 Sauti Ya Pwani 3 Sauti Ya Pwani KAUNTI YA KILIFI KAUNTI YA KILIFI Bustani ya mimea asilia yaanzishwa Pwani Na Irene Agum, Kaunti ya Kilifi ustani kubwa inayojumuisha aina zaidi ya 10,000 ya mimea asili ambayo ilianzishwa hapa Pwani kwa takriban shilingi milioni tano sasa imefunguliwa rasmi katika chuo kikuu cha Pwani kilichoko mjini Kilifi na kutoa changamoto wa mwanzo wa ubunishaji wa mazingira bora hapa Pwani. Bustani hii iliyobuniwa kwa ushirika wa Chuo cha Pwani, shirika la kitaifa la mazingira, NEEMA na Shirika la kimataifa la DANIDA litatumiwa kama ghala la kuhifadhia aina mbali mbali ya mimea kote duniani ikiwa ni pamoja na ile mimea inayotishiwa kuangamizwa. Bustani hii inatarajiwa kuwanufaisha wanasayansi na wachunguzi wa mimea na hali kadhalika kuwa kivutio cha watalii hasa ikiangaziwa mwelekeo wa kupandwa katika sehemu mbali mbali ikihusisha mimea inayofikiriwa kuwa na uwezekano wa kutibu magonjwa, kuwa na mbao bora, B aina ya mimea isiyokuwa ya kawaida, ile iliyo na manukato, vyakula na vile vile ile inayotumiwa kama vivutia macho. Kwa sasa mmea kama vile ‘vilua’ ambao unakuzwa kwa wingi hapa Pwani, unafanyiwa majaribio ili uhusishwe kwenye viwanda vya virembesho kutokana na ubora wa manukato yake. Bustani hii inatarajiwa kuwa na mimea aina nyingi zaidi hapa afrika. Nchi ya Kenya inakisiwa kuwa na aina zaidi ya 100 zinazoorodheshwa kama aina ya ‘aloe vera’ na ambazo zinavunwa kwa kasi kiasi cha kutishia kuangamizwa, kulingana na Dkt. Mohamed Pakiya ambaye ni mtaalam mkuu wa bustani katika Chuo kikuu cha Kilifi. Bustani hii pia inatarajiwa kubadilisha hali ya maandhari ya Kilifi kutokana kuletwa kwa aina ngeni za mimea kutoka sehemu nyingine za dunia. Uzinduzi wa bustani hii hapa Pwani ulioongozwa na kaimu mwenyekiti wa NEEMA, Bi. Kulamo Bullo ulikuwa chanzo cha kubuni mwongozo mahsusi wa maendeleo hapa Pwani. Mwongozo huu utawezesha ukufunzi wa mawazo na uchunguzi kunufaisha jamii moja kwa moja baada ya kuwajumuisha. Kulingana na msimamizi wa Chuo hicho, Profesa Mohamed Rajab, mwongozo huo unatoa mikakati ya utekelezaji ikiwa ni pamoja na mbinu za kuendeleza miradi na mipangilio katika chuo. Haya yanatarajiwa kuwa sambamba na mipangilio ya Chuo kama michango ya kuendeleza elimu kwa maendeleo ya kitaifa. Elimu kwa maendeleo ya kitaifa (ESD) ni mbinu zinazotumika kufundisha na kusoma zinazoegemea kujitegemea; jamii zinatarajiwa kubuni ari ya masomo, ujuzi na elimu ya kuendeleza bila kuvuruga vizazi vijavyo kujiendeleza.. HALISI COMMUNICATIONS Your professional Consultants in Printings, Video & Photo productions, Media, IT and Capacity Building. GOODS/SERVICES 1. DESIGN, TYPESETTING &PRINTINGS: T-shirts, Magazines, Newsletters, logos, posters, signboards, cards, receipts etc. 2. PRODUCTION: Video shooting & Editing for news, corporate affairs, weddings, ceremonies, documentaries etc. Photography & Digital Imaging; for all types of occasions and purposes. 3. EVENTS MANAGEMENT: Tents, chairs, sound systems, lighting, catering for HIRE. 4. SUPPLIES: Stationery, toners, cartridges, computers, laptops and accessories, tree seedlings and flowers, printed exams for primary & secondary schools. 5. TECHNICAL & MEDIA: IT solutions, computer repairs and maintenance, web designs and programming, news and features services for radio, TV, print and online publications and social media. 6. TOURISM: In partnership with Mlilo Community Tours& Safaris. Bookings, tour guiding, provision of camping sites home stays for ecotourism within rural communities. Video productions and photography for tourism experiences and promotions. 7. CAPACITY BUILDING: On-job, on-site and in-house trainings in community development issues, proposal writing, community tourism enterprises, internship for tourism and media students, project management, mentoring and motivational speaking. Network across East Africa- Kampala, Busia (U&K), Malaba, Kakamega, Mumias, Kisumu, Mwanza (Tz), Nairobi Malindi branch- Malindi-Lamu Rd. Contacts – Latifah Abdallah (Nidhamia Hall) -0707-956592 Musyoka A - 0710-335833 Bernard - 0710-996042 Livingstone - 0712-340875 Albert - 0724-539302 Kustawisha Uvuvi kazkazini mwa Pwani Na Irene Agum, Kaunti ya Kilifi h a b a w a s a m a k i unaosababishwa na vifaa vya uvuvi duni unadaiwa kusambaratisha juhudi za kuanzisha mitambo ya biashara ya samaki wa mikebe huko kazkazini mwa Pwani. Mitambo miwili iliyoko sehemu hiyo imekuwa ikifanyiwa kazi ndogo ndogo kwa vile wavuvi katika sehemu hiyo wameshindwa kuvua samaki wakutosha. Mitambo hiyo ikiwa na uwezo wa kusaga na kuhifadhi samaki tani 12,000 kwa siku katika kampuni ya Diamond Sea Food Limited inalazimika kufanya kazi kati ya mwezi wa Oktoba na Machi, ikisaga na kuhifadhi tani tano pekee ambayo haifikii hata nusu ya uwezo wa mitambo yake. Hii inatendeka katika sehemu iliyo na maeneo makubwa ya samaki ambayo yana uwezo wa kuipatia nchi hii zaidi ya shilingi milioni 75 kila mwaka. Wavuvi hata hivyo wameiomba serikali iwasaidie kuongeza viwango vyao vya kuvua samaki kwa kuwapatia meli kubwa zitakazowawezesha kuvua samaki kwenye maji marefu badala ya kutegemea kujenga mabohari. Wavuvi hawa wanasema kuwa mahitaji ya samaki yamekua kwa kiwango kikubwa hata baada ya kubuniwa kwa kilimo cha kufuga samaki na kuwa sehemu nyingi za uvuvi bado hazivuliwi. Akizungumza na vyombo vya habari huko Mtwapa, mkurugenzi mkuu wa Diamond Sea Foods Limited, Bw. Mohamed Khizer alisema wingi wa samaki katika maeneo yaliyopakana na Somalia kama vile Lamu, Malindi, Watamu na Kilifi imedhihirika lakini ukosefu wa meli za kuvulia umewafanya wavuvi kusalii amri na kushindwa kuendeleza uvuvi. Kwa sasa kuna meli moja tu yenye uwezo wa kuvua maji marefu. U Daktari wa macho akishughulikia moja ya wateja wake Afya ya jamii yakumbwa na matatizo ya usafiri Na Irene Agum, Kaunti ya Kilifi atizo la usafiri linaendelea kuwa k i k w a z o k i k u b w a kinachochangia kuzorota kwa afya ya jamii katika kaunti ya Kilifi. Barabara duni na vituo vya afya vilivyojengwa mbali vimesababisha wanawake wengi kuzalia majumbani mwao ilhali wengine wao hujitosa kwa waganga wa kienyeji ingawa wizara ya afya inafanya kila jitihada kuboresha huduma za matibabu kote nchini. Watu wengi wanaozuru zahanati kwa matibabu wana dhana kuwa wauguzi ni wale ambao bado wako mafunzoni na wanaaihimiza serikali kuwatuma wauguzi waliohitimu katika zahanati hizi za Kaunti ya Kilifi. Wanawake wanaonekana kuwa na wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa muda wa ‘uchungu’ wakati wa kuzaa ilhali wengine huwa wanapatwa na matatizo ya kubaki na ‘mji’ au nyumba ya mtoto jambo ambalo linachukuliwa kama mkosi baina ya wanawake waoga katika kaunti hii. Uchunguzi uliofanywa hivi karibuni umeonyesha kuwa itikadi na mila katika sehemu nyingi za kaunti ya Kilifi zimewafanya wanawake wengi kususia kupimwa kabla na baada ya kuzaa na badala yake kutegemea huduma za wakunga wa kienyeji. T Uchunguzi huu umependekeza kuwa wakunga wa kienyeji na wale wazazlishaji waliostaafu waruhusiwe kuendeleza huduma zao kwa vile wamekuwa wakitegemewa pakubwa kutokana na itikadi na mila zilizokithiri miongoni mwa wakaazi wa kaunti ya Kilifi. Uchunguzi huo uliofanywa na shirikia lisilokuwa la serikali, Kwetu, lilichukua muda wa miezi sita na limegundua kuwa gharama kubwa ya usafiri na umbali wa zahanati unawanyima fursa ya kupata huduma za matibabu. Uchunguzi huo ulidhamiriwa kutafuta chanzo cha kuzorota kwa idadi ya watu wanaopokea huduma za matibabu. Akipokea ripoti hiyo ya uchunguzi kutoka kwa afisa wa haki za binadamu, Bi. Joria Suud, mkuu wa matibabu wa Kilifi Dkt. David Mulewa alidokeza kuwa ingawa kuna changamoto nyingi kutokana na upungufu wa wauguzi amekuwa akiwahimiza vijana wengi walio na kisomo kujiunga na Taasisi ya matibabu (KMTC) ama Chuo kikuu cha pwani ambavyo vinatoa shahada za uuguzi hapo Kilifi. 4 Sauti Ya Pwani Tahariri KAUNTI YA LAMU UPOFU Huku ulimwengu mzima ukiadhimisha siku maalum iliyotengwa kuangazia kutunza macho, wenyeji wa kaunti ya Kilifi na vitongoji vyake hawana lolote lile la kufufahia kwa vile wanaendelea kukumbwa na matatizo ya macho. Kwa wale wachache ambao hujitahidi kusafiri mwendo mrefu ili wapate matibabu ya macho Katika hospitali kuu ya Kilifi ni kero kwani kuna daktari mmoja tu ambaye hutibu watu siku mbili tu kila wiki. Ukifika kwenye zahanati inayoshughulikia macho utakuta milolongo mirefu ya wagonjwa wa macho ambao wengi wao huambiwa waende kwa matibabu Katika hospitali kuu ya mkoa wa Pwani mjini Mombasa, ilhali wengine wamejulikana kuwa vipofu kwa ugonjwa ambao ungetibika iwapo wangemuona daktari wa macho kwa wakati ufaao. Kulingana na Dkt. David Mulewa ambaye ndiye mkuu wa matibabu Katika hospitali kuu ya Kilifi, huduma ya matibabu ya macho inakumbwa na uhaba wa madaktari waliohitimu taaluma ya macho na anawaomba washirika na wadau kujitokeza kuisaidia hospitali ya Kilifi kukabiliana na tatizo hilo. Kati ya maradhi yaliyopokewa Katika hospitali hii ni pamoja na viini vinavyosababisha upofu hasa Katika watoto; inakisiwa kuwa zaidi ya watu milioni 18 wamepofuka duniani ilhali ugonjwa huu una tiba. Inadaiwa kuwa watoto ndio walio kwenye hatari ya kuambukizwa na hivyo basi kuchangia kuendeleza umaskini baina ya jamii. Wakati wa kliniki ya bure iliyofanyika Katika kanisa la Katoliki la Kilifi, madaktari walionya kuhusu ugonjwa wa kisukari kama moja ya sababu zinazoleta upofu. Daktari mmoja wa macho kutoka Mombasa, Dorcas Njuguna anasema kuwa kisukari huambukiza mishipa ya macho na kumfanya mtu kuona vugu vugu na kuwa kipofu bila kutambua kwa vile haina maumivu. Ni dhahiri kuwa ugonjwa huu una madhara na wito wetu ni kuwahimiza wananchi kuhudhuria kliniki mara kwa mara ili wajijue hali zao za kisukari na macho ili janga hili liweze kuangamizwa. Athari za ukame zazua maafa Na David Mutwiri na Jackline Wambui, Kaunti ya Lamu aunti ya Lamu, kwa muda mrefu sasa, imekuwa kimbilio na mokozi wa jamii za wafugaji kutoka maeneo ya kazkazini mwa Kenya wakati wa kiangaza lakini maendeleo ambayo yanajiri kutokana na kuanzishwa bandari mpya yaonekana kukatiza maeneo ya malisho na hivyo basi kuzusha taharuki kati ya binadamu na wanyama, jambo ambalo limeshuhudia vifo vya watu wengi huku wengine wengi wakijeruhiwa. Taharuki ya binadamu na wanyama ilizidi na kufikia viwango vya kutisha baada ya vurumai za Tana Delta ambazo zilisababisha jamii kutorokea usalama wakiambatana na makundi makubwa ya mifugo na hivyo basi kuongezea uhasama ambao ulikuwa unasababishwa na jamii za kuhamahama kutoka wilaya jirani za Ijara. Hali hii inazidi kuwa mbaya kutokana na kubuniwa kwa maeneo ya ufugaji ambayo yamewawekea vikwazo na ku z i b a n j i a a s i l i a wa l i zo ku wa wakizitumia wafugaji wa kuhamahama. Baadhi ya maeneo haya ya ufugaji hayaeleweki, wala mipaka yake haijulikani na yanadaiwa kumilkiwa na mabwenyenye waliolenga upanuzu na maendeleo yaliyoletwa na ujenzi wa bandari ya Lamu. Maeneo ya kazkazini mwa Kenya yanajulikana kwa kukumbwa na janga ukame lakini shida ni kuwa bado hakujapatikana suluhu bayana kwa tatizo hili sugu. Eneo hili kame linalopakana na nchi jirani inayokumbwa na vita vya mara kwa mara ni makaazi ya jamii ya wafugaji wa kuhamahama ambao wana sifa za kufuga wanyama wengi ambao huwalazimu kuhama kutoka eneo moja hadi lengine wakitafuta K Uhamaji wa mara kwa mara wa wafugaji hawa umekuwa ukiendelea kutoka miaka ya sabini huku mifugo ikiingia Lamu kutoka maeneo jirani ya Garissa, Tana Delta, Bura na hata Ijara. Baadhi ya wafugaji hawa walikumbana na ubatili wa maendeleo mapya hivi majuzi wakati walipojaribu kuingiza mifugo wao kutoka Ijara na kukatazwa ikidaiwa kuwa maeneo hayo yalikuwa ni mali ya mtu binafsi. Jambo hili liliwafanya wafugaji hao kupoteza zaidi ya ng’ombe 40 baada ya kukosa malisho na maji kwa zaidi ya siku kadhaa. Huku suluhu kwa matatizo haya yakiwa kitendawili, wafugaji hawa wamejikuta kwenye njia panda na kukorofishana na wakulima ambao wanadai mifugo inawaharibia mimea yao. Wakati wa uhamisho, makundi makubwa ya ng’ombe hujaribu kunywa maji kwenye visima vilivyo katikati ya mashamba. Kwa makundi ni makubwa na wachungaji ni wachache, ng’ombe hugeukia mazao ya wenyewe na kusababisha uharibifu na kuzua farakano. Ni kati ya hali hizi zisizofurahisha kuendelea uk. Wa 5 13 Sauti Ya Pwani Mazuia maji yajengwa Pate na Ndau Na David Mutwiri, Kaunti ya Lamu haribifu wa vifaa na bidhaa unaosababishwa na mawimbi mazito ya Bahari katika maeneo kadha ya siwa la Lamu yatazikwa kwenye kaburi la sahau baada ya serikali kutumia zaidi ya shilingi milioni 364 kujenga mazuia na kuta katika visiwa vya Pate na Ndau. Mradi huo ulihusisha ujenzi wa ukuta wa mita 1400 kwenye kingo za Bahari za Faza katika kisiwa cha Pate na zuia la mita 420 katika kisiwa kidogo cha Ndau mashariki mwa kaunti ya Lamu. Mheshimiwa Chris Obure, ambaye ni waziri wa Ujenzi wa kitaifa alidokeza kuwa ujenzi wa kuta la Faza na lile zuia la Ndau ziko kwenye vitengo vya maendeleo viitwavyo “kazi nyingine za taifa” vinavyoshuhulikia ujenzi na ukarabati wa madaraja madogo, kuta za Bahari, vituo vya kuegesha madau na mazuia. “Hapo awali maji ya Bahari yalikuwa kero kwa vile wakati maji yanapojaa, mawimbi mazito yalikuwa yakisukumwa hadi ndani ya nyumba na kuharibu mali na kuwa kero kwa wenyeji wakati wanapotembea au kufanya kazi kwenye ufuo wa Bahari U wa Faza,” akasema Obure. Waziri huyu aliyasema hayo wakati wa hafla ya kupokea mradi wa Faza iliyofanywa hivi majuzi. Ujenzi wa kuta la Faza na lile zuia la Ndau zilianza kujengwa kuanzia mwezi wa Oktoba 2007 na ulitarajiwa kukamilika Agosti 2010. Serikali pia imetenga shilingi milioni 42 zitakazogharamia ujenzi wa kuta katika kijiji cha Kizingitini. Mradi huo utakaojumuisha njia badala ukingoni ya kilomita 1.35 sambamba na kikuta cha Ndau inatarajiwa kukamilika mwezi wa Julai 2013 kulingana na mhandisi wa wizara ya ujenzi, Mhandisi Benjamin Mwangi. Takriban mita 5,000 za kuta katika fuo za Bahari zimejengwa na kukarabatiwa katika kaunti ya Lamu toka mwaka wa 2003 ili kuchangia maendeleo ya kiuchumi na hasa mawasiliano ili kuwasaidia wenyeji kutimiza malengo ya riwaza ya kitaifa ya 2030. Ujenzi wa kuta za baharini unafaanywa na kampuni ya Associated Construction Company Limited ikisimamiwa na tume ya usimamizi ya wizara ya Ujenzi. Wizara hiyo pia itatumia shilingi bilioni 1.2 kukarabati kiegezo cha SAUTI YA PWANI EDITORIAL Ag. Editor: Hussein Abdullahi FIELD EDITORS Simon Guruba: Daniel Mwangi: Mercy Ndirangu: Irene Agum: Paul Olalo: Emmanuel Masha: Mutiso Mbithi: Wundanyi Voi Kwale Kilifi Malindi Hola Lamu PRODUCTION Safari Baya: Mariakani ADVERTISING RATES Full page Half page 1/4 page 1,000.00 600.00 400.00 Kambi ya muda iliyobuniwa kufuatia uvamizi huko Tana Delta. Jamii kadhaa zililazimika kukimbilia usalama baada ya uvamizi uliosababisha maafa na majeruhi KAUNTI YA LAMU madau ili kuboresha biashara za utalii katika sehemu hiyo. Habari zaidi zasema kuwa Wizara ya ujenzi inanuia kufanya michoro ya kiuhandisi itakayokuwa na mitindo sawa kwa mijengo yote ya makao makuu ya kaunti kote nchini ili kuwe na usawa katika ugavyi wa mamlaka ya serikali. Waziri Obure huku akitoa agizo kwa mchoraji rahamani mkuu katika wizara yake kuhusu mtindo wa majengo yatakayoptumika kwa wakuu wa kaunti, alisema kuwa anafadhaishwa na jinsi wizara nyingine zinavyojenga maofisi kiholela bila kushauriana na wizara yake. Obure, ambaye alikuwa amemtembeelea Mkuu wa Kaunti ya Lamu, Stephen Ikua alisisitiza kuwa wizara yake itahakikisha kuwa kuna usawa wa mitindo ya majengo ya afisi zote nchini na kuhakikisha kuwa yamejengwa kwa viwango vya juu vya kuridhisha ugatuzi. “Nikiwa kwenye wizara iliyopewa jukumu la upangaji, uchoraji, ujenzi na hata kukarabati rasilimali za serikali, nitajitahidi kuhakikisha kuwa mahitaji ya miundo misingi ya ujenzi katika kila kaunti inatimizwa ili kukuza uchumi wa kitaifa,” akasema Mhe. Obure. Waziri huyo alidokeza kuwa wizara yake imesimamia ujenzi wa zaidi ya majengo 750 ya wizara mbali mbali humu nchini na pia kukarabati miradi zaidi ya 222 kupitia kwa kitengo cha wizara yake kinachosimamia uboreshaji na ukarabati wa majengo ya serikali. “Wizara yangu pia imesimamia ujenzi unaohusisha sekta mbali mbali kama vile mashule, hospitali, sekta ya kilimo na kukamilisha majengo 210 kati ya 226 yaliyokuwa yamekwama katika sehemu mbali mbali humu nchini,” akaongeza Bw. Waziri. Alitangaza kuwa wizara yake itatenga zaidi ya shilingi milioni 30 kugharamia ujenzi wa makao makuu ya Faza katika kaunti ya Lamu. 12 Sauti Ya Pwani 5 Sauti Ya Pwani KAUNTI YA TAITA-TAVETA KAUNTI YA TAITA-TAVETA Wafugaji watahadharishwa kujiandaa kwa ukame Na Wagema Mwangi, Kaunti ya Taita Taveta dara ya Ufugaji wilayani Mwatate katika Kaunti ya Taita Taveta imetoa tahadhari huenda kukawa na ukame wa muda mrefu baada ya mabwawa kukauka kufuatia kiangaza kikali. Maeneo mengi katika wilaya hii inayojulikana kuwa eneo kame, kwa muda wa miezi mitano iliyopita imekumbwa na uhaba wa maji hali ambayo imesababisha kumalizika kabisa malisho katika eneo la malisho. Huku mifugo wadogowadogo wakiendelea kustahamili, afya za wale wakubwa kama vile ng’ombe zinaendelea kuzorota na kutoa tisho huenda wafugaji wakapata hasara kubwa kutokana na maafa ya mifugo wao. Akizungumza na mwandishi wetu, afisa mkuu wa mifugo wa wilaya ya Mwatate, Bw. Martin Oyindo alisema kuwa sehemu zilizoathirika zaidi ni pamoja na Mwakitau, sehemu za Mwatate na Kamutonga. Alisema kuwa mvua ambazo zimekuwa haziaminiki toka mwezi wan ne imesababisha nyasi kukauka kwenye maeneo kadha ya malisho na hivyo basi kuwafanya wafugaji kuwa na fedheha kwa mipangilio ya siku za usoni. “Tuna wasi wasi mkubwa kuhusu mifugo wetu kwa siku zijazo. Mabwawa yote sasa yamekauka ilhali mvua nazo bado hazijaanza kunyesha kama tulivyotarajia,” akasema Bw. Oyindo. Afisa huyo aliwashauri wafugaji walio na makundi makubwa ya mifugo wachukue hatua za haraka za kuwauza huku masoko yakiwa na bei nzuri na akasisitiza kuwa ni bora kuwa na mifugo wachache ambao watawashughulikia vyema wakati I huu wa kiangaza. Alidokeza kuwa wafugaji wamekuwa wakiwapoteza mifugo wao wakati wa kiangaza na akaonya kuwa hali hiyo itajiri iwapo wakulima hawatachukua hatua za haraka kuwapunguza mifugo wao. “Ni lazima tuwauze mifugo wetu wa ziada ili tuepuke kupata hasara. Tutakuwa na fursa ya kununua wengine wakati mvua inyeshapo," akasisitiza. Hali hii ya upungufu wa mvua inazidi kuwa mbaya, kwa vile inawalazimu wenyeji kufunga safari ndefu wakitafuta maji kwa matumizi yao na vile vile kwa mifugo wao na mara nyingi kuuziwa kwa bei ghali mno. Idara ya hali ya anga ilikuwa imetoa tahadhari kuwa huenda kukawa na mvua nyingi kuanzia mwwezi wa Oktoba lakini hali hii bado haijaonekana katika sehemu kadha za nchi. Fika Mnarani, Kilifi kwenye makavazi uone moja la pango la watumwa Kondoo mweusi atimuliwa kanisani Na Salome Mbeyu Tsuma- Kaloleni K ijana mmoja ametimuliwa na mchungaji kanisani, kwa kukosa kujirekebisha kutokana na ‘mrundiko wa dhambi’. Mchungaji George Tsuma, wa kanisa la Rehoboth Fellowship katika kijiji cha Chandoni wilayani Kaloleni, alimtimua Collins Lisambu, mwenye umri wa miaka 19, kwa madai ya wizi na ulevi, miongoni mwa mengine. Katika tukio la hivi karibuni, Lisambu anasemekana, aliiuza pikipiki ya muumini mmoja wa kanisa hilo, baada ya kumwomba kutumia. Mchungaji huyo alisema kadhalika waumini walichoshwa na tabia yake ya kuja kanisani akiwa mlevi, kuwatongoza wasichana pale, na kuhusishwa na visa kadhaa vya wizi. ‘Alikuwa fedheha kubwa kwa kanisa kwa sababu kila mara anaposhikwa na polisi kuhusiana na uhalifu, sisi ndiyo tunaotoa faini kumaliza mambo hayo. Sasa akishikwa kanisa halitahusika’, alisema Tsuma. Shirika la Huduma za Wanyama Pori kuimarisha elimu Taita Na Simon Guruba, Kaunti ya Taita Taveta hirika la huduma za wanyama wa pori (Kenya Wildlife Service) limetumia takribani shilingi milioni thamanini (sh80million) kufadhili miradi ya elimu tafauti tafauti katika Kaunti ya Taita Taveta ili kuinua viwango vya elimu katika eneo hili. Miradi hii ni kama Mwaktau youth polytechnic, Kiangachini nursery school, Manyani, Mwamunga, Mulilo primary schools na madawati kwa shule ya msingi ya Kishushe. Pia mwaka wa 2004 shirika la KWS lilifadhili ujenzi wa madarasa mane, afisi ya mwalimu mkuu na chumba cha walimu (staffroom) katika shule ya upili ya Mwaktau. Akianzisha rasini ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Mwakitau ambalo ligarimu shilingi milioni mbili nukta inne (sh2.4m) na kufadhiliwa na shirika la huduma za wanyama wa pori, naibu wa mwenyekiti wa bodi la huduma la udhamini la wanyama wa pori (KWS Board of Trustee) ambaye pia ni mkurugenzi katika bodi hiyo Bi. Margaret Mwakima alisema shirika la KWS limejitolea kuinua kiwango cha elimu na maisha ya jamii za Taita Taveta Kauti. Akiongea hapo shuleni hivi majuzi Bi. Mwakima alisema shirika la KWS linafahamu kwamba masomo katika kata za Mwaktau na Mwachabo hutatizwa sana na ndovu wakati wanapo vamia sehemu hizo. Akihutubia wazazi na wanafunzi wa shule hiyo Bi. Mwakima alisema ili kuhakikisha kwamba Kaunti ya Taita Taveta inashindana vyema kielimu na maeneo mengine nchini, shirika la KWS litahakikisha kwamba visa vya uvamizi ambavyo vinatekelezwa na ndovu ama wanyama wote wa porini vinamalizwa. Hali hii itaweza kuinua kiwango cha elimu na kuhakikisha wanafunzi wanaendelea na masomo yao shuleni bila kutatizwa na ndovu kwa kuwazuia ndovu kuwavamia kupitia ujenzi wa uwa S wa umeme. Bi. Mwakima anasema “shirika la KWS linasikitika sana kuona baadhi ya shule hupunguza masaa ya masomo wakati wanafunzi hu lazimika kufika shule kuchelewa ama kurudi nyumbani mapema kuhofia uvamizi ama kushambuliwa na ndovu”. Pia Bi. Mwakima alisema lengo la shirika la KWS kujenga bweni katika shule ya Mwaktau kutapunguza visa vya wanafunzi kushambuliwa na ndovu wakati wakitoka nyumbani kwenda shule kwani watakuwa wanabaki shuleni. Anasema visa nya “watoto wa shule kukosa kuendelea na masomo ya shule za upili kwa sababu shule hizo ziko mbali na upungufu wa wazazi ama kushidwa kwao kuwapeleka watoto shule vitapungua kwani shule ya bweni iko karibu”. Kwa wanafunzi, Bi. Mwakima alisema ufanisi kwa masomo hayatokani tu kupitia kwa majengo mazuri, walimu wakutosha na vitabu bali pia kunatokana na kiwango cha umasikini katika jamii, afya ya wanafunzi, mchango wa wazazi kwa elimu ya watoto wao na pia uhusiano wa wanafunzi kwa wanafunzi shuleni. Alisema tabia kama uhusiano wa kimapenzi kati ya wanafunzi wasichana, ndoa na mimba za mapema na unywaji wa pombe kwa baadhi ya wanafunzi vimechangia kud- horora kwa kiwango cha elimu katika Kaunti ya Taita Taveta. Pia aliwahimiza wazazi wajihusishe na masomo ya watoto wao, waunge mkono miradi ya elimu na kupitia kwa juhudi hizo visa vya watoto kuacha shule vitapungua na kuinua kiwango cha elimu katika Kaunti hii. Athari za ukame Kutoka uk. Wa 4 ambapo wafugaji wa jamii za kisomali na wakulima wa kaunti ya Lamu walikutanishwa kwenye mkutano wa amani hivi majuzi. Hapo, Mkuu wa kaunti hii, Stephen Ikua alikiri kuwa nyakati zimebadilika na hali ya maisha pia zimebadilika. “Maeneo makubwa ya malisho sasa hayako tena kutokana na ongezeko la watu jambo ambalo limezua vizazi vipya na ongezeko la mifugo,” anasema Bw. Ikua. Upungufu wa maeneo ya malisho, anaongeza Bw. Ikua, yataendelea kupungua zaidi hasa kutokana na ujenzi wa bandari na kubuniwa kwa mji mpya wa kisasa. Dalili za kupanuka kwa mji wa Lamu, umewavutia wawekezaji wengi ambao wanajaribu kukita mizizi ya biashara zao wakijiandaa na yajayo ili wapate faida. Wanafunzi wakiandaliwa kwa zoezi la kilimo bora 6 Sauti Ya Pwani 11 Sauti Ya Pwani KAUNTI YA MOMBASA KAUNTI YA MOMBASA Lamu na utamaduni wake Lamu: Mji ulojawa na utajiri wa utamaduni, historia na mila Na Nyambura Ngugi, Kaunti ya Mombasa wa muda mrefu, mji wa L a m u a m b a o umeorodheshwa na shirika la kimataifa la UNESCO kama kitovu cha utajiri wa utamaduni, historia na mila za jadi, umeendelea kuwa kivutio kikuu kwa wageni kutoka sehemu mbali mbali humu nchini, hali kadhalika wale wa kimataifa huku kisiwa hicho kikitoa maandhari ya kufurahisha na kuburudisha kimaisha. Barabara nyembamba, vichochoro na kingo za bahari zilizojaa watalii na wenyeji waliovalia mavazi yaliyoegemea tamaduni za kiislamu limekuwa jambo la kawaida. Hali hii ya utajiri wa mila na desturi, historia na majengo ya jadi ya Kiswahili inajiri mjini Lamu kutokana na wageni walioitembelea katika karne za 13 wakiwemo Wareno na Warabu. Hata hivyo, baadaye makundi mengine yakitalii yalijitokeza na kuhamia mjini humo na kuingiza tumbo joto utajiri huo baada ya kuingiza desturi mbovu kama vile utumiaji mihadarati, ukahaba na hata ushoga. Ingawaje Lamu ni eneo linalomilkiwa na waislamu ambamo desturi hizo zinalaaniwa na makundi yote ya watu wakiwemo wakristo, wenyeji na hata wageni wanaoishi humo, desturi hizi zimekuwa zikiendelezwa pasipo kujali, kwani huendelezwa kisiri ili watu wasijue. Tukitaka kufichua jinamizi hili, mwandishi huyu alisafiri hadi kisiwani Lamu, akachunguza kwa kina na marefu na kutuandalia taarifa hii maalum kuhusu ushoga. Kutana na Simon, silo jina lake, lakini akiwa mfanyi kazi anayewaelimisha mashoga na mabasha (watu wanaofanya mapenzi na wenzao wa jinsia moja-MSMs) katika zahanati ya hospitali kuu wilayani humo, amejitolea kwa hali na mali kufunza njia salama zakutumika wakati wakufanya ngono. Hakudhania kuwa kazi hiyo inge K hatarisha maisha yake kwani miezi michache iliyopita, kundi la wanakereketo waliivamia hospitali ya Lamu kwa kuandaa warsha iliyonuiwa kuwalenga mashoga jambo ambalo lilidaiwa kuwa kinyume na maadili ya wenyeji wa Lamu na ambalo lingeendeleza jinamizi la ukahaba na ushoga. Simon anasema kuwa ingawa jamii kubwa ya wakazi wa Lamu ni waislamu, ukweli ni kuwa haijakubalika kuwa mashoga na mabasha ni binadamu wanaoishi miongoni mwetu na kama raia wengine wana haki ya kikatiba kupata mahitaji ya kimatibabu ya kimsingi. Simon amekuwa akijihusisha zaidi na kuzuia kusambaa kwa UKIMWI na kuwatunza waadhiriwa katika kaunti hii na katika muda wa miaka mitatu sasa, amekuwa akiwahamasisha wenyeji kuhusu kufanya mapenzi wakitumia kinga na kupimwa mara kwa mara ili wajue hali zao kiafya. Kulingana na takwimu za hospitali hiyo, asili mia nne za watu huathirika lakini huwa inaongezeka au kupungua kutegemea wingi wa wageni wanaoingia na kutoka Lamu. Mila na desturi zinazokashifu ushoga zimekuwa changamoto hasa ikizingatiwa utoaji huduma za matibabu kwani mashoga ndio walio na idadi kubwa ya waathiriwa wa UKIMWI, Simon alimwambia mwandishi huyu kwenye majadiliano ya moja kwa moja. Imemchukua Simon zaidi ya miaka miwili kukubalika na kujumuika na mashoga kama mwalimu kuhusu kinga na ngono. Afisa huyu anadai kuwa viongozi katika eneo hili hawajihusishi kikamilifu kuendeleza mbinu za kuzuia kusambazwa kwa UKIMWI na hali hii imeifanya kazi yake ya mafunzo kwa wakaazi kuwa ngumu zaidi. Ongezeko la ngono baina ya watu wa jinsia moja limeongeza viwango vya kuvunjika ndoa na watu wanapojiingiza kwa ndoa nyingine huchangia pakubwa uenezaji wa UKIMWI kisiwani Lamu, anasema afisa huyo. Kutokana na hali hii, viongozi wa Inaendelea uk. Wa 11 Vijana wajitokeza kujiunga na shirika la huduma za vijana Chapati yazusha Kizaazaa Na Paul Olale –Kilifi Kaunti ulitokea kizaazaa wakati jamaa mmoja aliibiwa chapati Na mwenzake katika kituo cha kuuza pombe ya mnazi, mtaa Maweni Mjini Malindi. Wakati(jina la utani) alipotaka kuondoka karibu saa tatu usiku, alipigwa na butwaa kugundua kwamba chapati haikuwepo kando yake kwenye kiti. Kisha alimwarifu Rukia, mwenye kituo hicho cha mnazi (mangwe), amsaidie kuitafuta. Alisemaamemuomba rafikiye amnunulie chapati hiyo, ili ampelekee mtoto wake upande mtaaKisumu Ndogo, kama chakula chake cha usiku. Lakini wateja walipoulizwa juu ya jambo hilo, hakuna aliyetoa habari yoyote. Basi Rukia aliufunga mlango wa kibanda hicho, na akawaagiza mababe wawili wawapekuena wanawake walio kuwa wakinywa pombe pale ndani. K Afisa wa Shirika la huduma kwa Vijana akikagua mmoja ya vijana waliojitokeza Lakini upekuzi huo kwenye mifuko, ndani ya nguo na chini ya viti, haikufua dafu. Kisha jamaa mmoja alitoa wazo kwamba watu wote wasimamishwe kutoka kwa viti vyaowote waliposimamishwa, Looo! Chapati uliofungwa kwa gazeti ulionekana kitini, ambapo kulikuwa kumekaliwa naFagia (jina la utani). Fagia alizomewa vikali na wateja kwa tukio hilo, lakini akadinda kuwa hakuhusika na kupotea kwa chapati hiyo. Lakini alipokuwa akidinda, hakuwa na habari kwamba kulikuwa na ushahidi zaidi ya kumhusisha; jamaa mmoja alimulika kwa tochi suruali yake, na sehemu ya makalio kulikwa na baka la mafuta! Agwambo alipandwa na hamaki, na akairaruararua ile chapati na kisha kuikanyakanyaga mavumbini, na akachomoka pale na kutokomea gizani. Kutoka uk. Wa 6 kidini wamehusishwa na wanapewa mafunzo maalum katika hospitali kuu ili wasambaze umuhimu wa kupimwa kabla ndoa na elimu hii pia inasambazwa kwa maharusi kupitia kwa viongozi wa kidini kabla ndoa kufungwa. Kwa vile mashoga wengine ni watu ambao wameoa na wana familia, afisa huyu huwa anaandaa vikao vya siri katika hospitali ili kuwapa mafunzo kuhusu kufanya ngono wakitumia kinga. Vikao kama hivi vinadaiwa kuhudhuriwa na zaidi ya watu ishirini ingawa kuna duku duku kuwa huenda wengi wao wamejificha baina ya jamii na hivyo basi kukosa huduma hii. Mashoga, kulingana na afisa huyu, wamepangwa kimakundi kwa minajili ya kutekeleza majukumu kama vile kugawanya mipira ya kinga wakati wa ngono, kutangazia raia umuhimu wa kupimwa UKIMWI na vile vile kuonyesha jinsi mipira ya kike na ile ya kiume inavyotumiwa. Ili kuwakinga na kejeli kutoka kwa wenyeji mashoga hawa wamefunzwa kuulaani ushoga na kuficha matendo yao halisi ili wawashawishi wenzao kuwa kamwe hawashiriki kwenye vitendo hivyo, Bw. Simon akamueleza mwandishi huyu. Hata hivyo, mbali na kukejeliwa, changamoto inayowapata ni pamoja na upungufu wa mafuta ya kulainisha, ukosefu wa matibabu wakati wanapoambukizwa hali kadhalika ukosefu wa ajira kwa vile wengi wao hawana kisomo wala vyanzo vya kuwawezesha kuanzisha biashara. Mmoja wa mashoga hawa aliyekiri kushiriki biashara hiyo alisema kuwa alijikuta kisiwani Lamu akiwa ametoka kwao, Nairobi. Alijitambua kuwa na jinsi za kishoga alipokuwa na miaka 12. Anadokeza kuwa wateja wake mara nyingi ni wageni na hata watalii ambao hutembelea Lamu kutoka sehemu mbali mbali. Wengine ni watu walio na familia zao hapa hapa mjini Lamu. “Niliweza kuwatambua wakati wa uvamizi wa hivi majuzi,” akasema. Yeye huwa anakumbwa na matatizo ya kuambukizwa magonjwa ya zinaa, na anapokumbana na mteja anayetumia madawa ya kulevya, basi huwa anapewa kichapo mara nyingine bila malipo. 10 Sauti Ya Pwani 7 Sauti Ya Pwani KAUNTI YA KWALE KAUNTI YA KWALE Viongozi wataka amani idumishwe Kwale Wakulima wataka pembejeo zipelekwe karibu zaidi Na Khamis Mohamed, kaunti ya Kwale iongozi wawaomba wananchi wa tarafa ya Kubo katika kaunti ya Kwale kudumisha amani wakati wa kampeni na uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwezi Machi mwaka ujao. Akizungumza katika baraza huko Shimba Hills, kamishna wa kaunti ya Kwale Bw. Evans Achoki aliwataka wakaazi kudumisha amani katika sehemu hiyo kabla ya uchaguzi na hata baada ya matokeo ya uchaguzi huo kutangazwa. “Nawataka mudumishe amani katika uchaguzi na hata baada ya uchaguzi nigependa mudumishe amani.” Alisisitiza Bw. Achoki. “Na amani huanzia na mtu nyumbani kwake. Kwa hiyo, ukishindwa kudumisha amani katika nyumba yako, huwezi kulalamika ukosefu wa amani katika jamii.” Aliongezea. Vile vile, Achoki aliwataka wananchi kushirikiana na vyombo vya usalama na kuripoti mtu yeyote yule watakeyemshuku kuwa huenda Na Khamis Mohamed, kaunti ya Kwale akulima wa maeneo ya Shimba Hills waitaka serikali kuwapelekea mbolea hadi mashinani karibu na mkulima ili wapate afueni kutokana na kulipa gharama za usafiri. Akiongea katika baraza huko Shimba Hills, Eliakim Muoka, mwenyekiti wa wakulima katika sehemu hiyo aliishukuru serikali kwa juhudi zake za kuhakikisha kuwa wakulima wa Shimba Hills pia wanapata pemebjeo. Vile vile, Muoka aliiomba serikali kuhakikisha kuwa pembejeo, haswa mbolea, inapatikana karibu na mkulima ili kumuondelea mzigo wa gharama ya kuisafirisha mbolea hiyo kutoka mji wa Kwale hadi Shimba Hills. “Mbolea ni pembejeo muhimu kwa kila mkulima na hatuwezi kuwa na usalama wa chakula bila ya kutumia mbolea. Kwa hiyo tuna imani kuwa afisi yako itatusaidia kwa hilo.” Muoka alimwambia kamishna wa kaunti ya Kwale, Evans Achoki aliyekuwa mgeni katika baraza hiyo. Katika wakati ambapo taifa la Kenya linajitayarisha katika kuupokea utawala wa ugatuzi, Muoka alifichua kuwa hatarajii kuwaona wakaazi wa wilaya ya Kwalewakipiga foleni wakipokea chakula cha msaada wakati serikali hiyo itakapochukua hatamu. Vile vile, aliomba kuboreshwa kwa soko la Mvindeni V akawa ma mpango wa kuvuruga amani ili hatua za kumdhibiti ziweze kuchukuliwa katika wakati unaofaa. Kamishna Achoki, alitambua elimu kama nyenzo ya kuhakikisha kuwa jamii inapata amani na hivyo basi, aliwahimiza vijana kujiendeleza kielimu hadi katika daraja ya chuo kikuu. Zaidi, aliwakanya na tabia ya kuacha masomo katika darasa la nane huku akizidi kuwahimiza pia kutafuta ajira ili kujikimu kimaisha. Afisaa huyo wa utawala aliwaomba wazazi nao kuipatiliza amani iliyopokuwapeleka watoto wao shule ili waweze kuja kuwafaidi katika maisha yao ya baadaye huku akitambua kuwa bila amani watoto hawawezi kuenda shule na kupata elimu. Kamishna huyo pia alifichua kuwa tarafa ya Kubo imekaa kwa mda sasa bila kuwepo na mkuu wa tarafa. Hata hivyo, alizidi kufichua kuwa serikali ipo mbioni katika kuajiri wakuu wapya wa tarafa ili kujaza nafasi zilizo wazi nchini. Ziara ya kamishna wa kaunti katika tarafa ya Kubo iliwasilisha bishara njema kwa wakaazi kuwa watapata mkuu mpya wa tarafa hivi karibuni. Vile vile, mwenyekiti wa kamati ya amani na maridhiano katikaya Kwale, Bw. Jackson Kaume naye aliiomba jamii kudumisha amani haswa katika mda huu ambao nchi ya Kenya ipo katika kipindi cha mpito. Kaume alisema kuwa sababu kubwa inayochangia katika kuvuruga amani katika maeneo ya Shimba Hills ni mzozo uliopo baina ya binadamu na wanyama pori jambo ambalo limekuwa mazoea kwa muda. Kaume alisema kuwa ndovu wamesababisha watu kuhama makaazi yao wakihofia kushambuliwa na wanyama hao. Vile vile, Kaume alizidi kuwaomba wanaohusika na kulinda wanyama pori kuwajibika katika kuona kuwa kuna maisha ya amani kati ya binadamu na wanyama pori wanaoishia katika mbuga ya wanyama ya kitaifa ya Shimba Hills. W ambalo lilijengwa na baraza la kaunti ya Kwale ili wakulima wapate kufaidika zaidi. Katika baraza yiyo hiyo, kamishna Achoki aliyasifu mazingira ya Shimba Hills akisema kuwa sehemu hii ina uwezo wa kupata mavuno ambayo yanaweza kuipiga marufuku njaa katika maeneo hayo. Pia, alitambua kuwa mbinu bora za kilimo ndizo zitakazowafanya wakulima kupata mavuno mengi na kujikomboa kutokana na hatari ya kukumbwa na baa la njaa. Kamishna Achoki pia alitambua hima ya wakulima katika kutaka kuimarisha kilimo chao kwa kutumia mbolea. Hata hivyo, alisema kuwa hata yeye anaunga mkono mapendekezo ya wakulima kuhusu kutaka kuondolewa mzigo wa kusafirisha mbolea toka Kwale hadi Shimba Hills. “Niko tayari kutilia pondo juhudi za kuimarisha kilimo katika maeneo haya kwani natambua juhudi zenu mnazozitia katika kilimo ili kuzalisha chakula Shimba Hills” alisema. Fauka ya hayo, kamishna huyo aliwatambua ndovu na wanyama pori wengine kuwa ndio wanaokwaza juhudi za wakulima katika kupata mavuno ya kutosha katika sehemu hiyo. Kila mwaka, wakulima hupoteza mimea na mazao yao kutokana na uharibifu wa wanyama pori. Stage View Café At Kinango Petrol Station—Kinango town Serves all types of: Cuisine, Nyama choma, Kuku choma and Fresh juice is also available Eat in comfort at our cool open air premises We offer outside catering services Kiegezo cha kisasa cha kusimamia meli. Kitapanua biashara ya uvuvi wa samaki Katika kaunti ya Kilifi na Pwani kwa jumla 8 Sauti Ya Pwani Ahitaji msaada kugharamia uuguzi Kutoka uk. Wa 1 Abdalla, ambaye ana umri wa miaka 36, mwanzo kabisa alianzwa na ishara za ugonjwa huu kwenye mguu wake wa kushoto lakini ugonjwa huu ulienea kwa haraka hadi sehemu za juu ya mguu huo. Ishara zinazidi kuonyesha kuwa huenda ugonjwa huu ukasambaa hadi kwenye mguu wake wa kulia ambao tayari umeanza kufura pia. Abdalla ambaye alikuwa mwelekezaji watalii, alilazimika kuwacha kazi hiyo kutokana na jinamizi la ugonjwa jambo ambalo lilimzidishia matatizo ya kumudu gharama za matibabu na zile za kulisha jamii yake. Akizungumza na waandishi wetu, Abdalla alidokeza kuwa alijigundua kuwa na matende siku moja alipokuwa akila chakula cha mchana na rafiki zake kwenye mkahawa. Kisha akahisi maumivu makali na kwa ghafla kupoteza ufahamu. Akapelekwa hospitali. “Nililazwa katika hospitali kuu ya Msambweni kwa siku tano. Hapo ndipo nilipogundua kuwa na matende baada ya kuchunguzwa na madaktari,” akawaeleza waandishi hawa.Abdalla alipelekwa kwenye Kituo cha uchunguzi wa matibabu cha KEMRI huko Kwale ambako uchunguzi zaidi wa kina ulifanywa na hata akawekwa kwenye mradi wa kuchunguza wagonjwa wa aina yake ambapo alikuwa akipewa vidonge vitatu kila mwaka. Alijitosa kwenye biashara za matatu kama manamba lakini hali yake ya afya ilizidi kuzorota, huku akihisi maumivu mengi kila uchao na uvimbe nao ukiongezeka kwa kasi zaidi. Ilimlazimu kuwacha kazi kabisa kwa hangeweza kusimama kwa masaa mengi kama inavyohitajika katika kazi za manamba, na akaanza kuwa mtu wa kutegemea wasamaria wema, majirani, ndugu na marafiki ili kumudu maisha. Abdalla ana matumaini ya kuishi maisha bora hata baada ya kuukata ule mguu mbovu kwani atakuwa na uwezo wa kutembea kwa urahisi akitumia mguu mmoja badala ya mzigo na maumivu anayoyapata kwa sasa inayosababishwa na mguu huwo. Hata hivyo inadaiwa kuwa madaktari katika hospitali kuu ya Msamb- weni wamedinda kumkata mguu ilhali madaktari wa KEMRI nao wamemshauri apate matibabu maalum jambo ambalo kwake ni ndoto kwa sababu ya ukosefu wa pesa licha ya hata zile za kujimudu yeye na jamii yake. Hivi majuzi tu, jamii na marafiki walikusanya shilingi 14,000 na kuwasaidia kwa sababu hata mkewe, Asha, pia hana ajira ilhali anatarajiwa kuwatunza wana wao wawili. Kijana wao wa kwanza, Abubakar, mwenye umri wa miaka 12 na aliye darasa la nne, alibahatika kuwa na mwalimu mkuu aliyemruhusu kuendelea na masomo ingawa hakuwa na karo. Hata hivyo kijana wake wa pili ambaye ana umri wa miaka sita na ambaye yuko kwenye shule ya vidumbule alifurushwa kutokana na ukosefu wa karo. Kwa vile yeye ni wa pili kupatwa na ugonjwa huo katika kijiji chake, Abdalla amekuwa akipata kero hasa akiona watu wakimtenga kwa sababu ana matende. Abdalla amejaribu kuficha mguu wake ambao mara nyingi huwa umezibwa na suruali ndefu na pana; Na ana desturi ya kuvaa viatu, lakini hivi havikuweza kupoteza kuchechemea kutokana na uzito na maumivu ya mguu. Kulingana na kumbukumbu za shirika la afya ulimwenguni, (WHO) za Januari 2012 zaidi ya watu bilioni 1.3 katika nchi 72 wanatishika kupatwa na ugonjwa wa matende, ugonjwa ambao inadaiwa umepuuzwa. Asilimia 65 ya watu walioambukizwa wanaishi kwenye eneo lililochaguliwa na WHO kusini mashariki mwa bara Asia, asilimia 30 wako hapa Afrika na asilimia zile zilizobakia ni wale walioambukizwa katika maeneo mengine duniani. Zaidi ya watu milioni 120 hapa Afrika na Asia kwa sasa wanaugua matende; huku zaidi ya watu milioni 40 wakiwa wameharibika viungo na hawaishi maiasha ya kawaida kutokana na athari za matende, kumbu kumbu hizo zinafafanua. Inasemekana kuwa matende kwa kawaida huambukizwa wakati wa ujana lakini dalili zake hujitokeza baadaye huku uvimbe ukijitokeza Inaendelea uk. Wa nyuma 9 Sauti Ya Pwani HABARI KWA PICHA Ukiukaji wa haki za watoto waangaziwa V Tafakari baada ya vurumai Tana Delta Kina mama na watoto waliathirika zaidi wakati wa machafuko ya Tana Delta Wakiwa wamekusanyika, wake kwa waume wakitafakari kwa kwenda baada ya mashambulizi Tana Delta Na Emmanuel Masha, Kaunti ya Tana River isa vinavyozidi kuongezeka vya kuvunjika kwa ndoa b a i n a ya j a m i i ny i n g i zinazoishi katika Kaunti ya Tana River ndivyo vinavyochangia ongezeko la watoto wasiokuwa na malezi bora, afisa mmoja wa watoto amenukuliwa na vyombo vya habari. Bi. Maria Ngali ambaye ni mkuu wa watoto wilayani Tana River anasema kuwa visa vya watoto waliopuuzwa visivyopungua sita huripotiwa kila siku kwenye afisi yake lakini akaongeza kuwa mtindo huo umwetapakaa kote katika Kaunti nzima. Bi. Ngali anasema kuwa kati ya Julai mwaka jana na Februari mwaka huu afisi yake ilikuwa imepokea zaidi ya visa 310, ikiwa visa 237 ni vile v i l i v yo ku wa n a u h u s i a n o n a kupuuzwa kwa watoto na akawaotea kidole cha lawana wanaume. “Wanaume wengi hapa wilayani hujiepusha na majukumu ya kijamii, hasa baada ya kuwataliki wake zao,” akasema kwa masikitiko. Akiongea na waandishi wa habari, Bi. Ngali aliyeandamana na afisa mwenzake, Bw. Daniel Wailti, aliwahimiza viongozi katika sehemu hizi, wazazi na maafisa wa serikali kushirikiana na kuhakikisha tabia hizi zinakoma. “Watu wengi katika sehemu hii ni wale wa dini ya Kiislamu ambayo haikatazi talaka. Wakati wazazi wanapotalakiana, ni bayana kuwa watoto huwa kwenye hatari ya kupuuzwa aitha wawe watakaa na baba au mama,” akasema. Katika muda huo huo, akadokeza afisa huyo, afisi yake ilipokea visa vya wafungwa 27, 12 vyake vikihusiana na utundikaji mimba ilhali visa tisa vilikuwa vya kupuuzwa kwa watoto. Visa vingine vilivyoripotiwa wakati huo ilikuwa pamoja na visa vitano vya watoto wenye mahitaji na wanaotaka malezi bora, visa vine vya wazazi waliokatazwa kuwaona watoto wao, na visa vitatu vya watoto walio na mahitaji ya karo, yatima na kuwachwa. Kwa bahati nzuri kuliripotiwa kisa kimoja tu cha ndoa za mapema ingawa kuna habari ya ongezeko la watoto kulazimishwa kuolewa hasa kwa jamii za kuhamahama. Afisa huyu alidokeza kuwa visa hivi huwa haviwafikii kwa vile vinashughulikiwa na jamii pamoja na viongozi wa kidini a m b a p o wato to wa h u s i ka huozwa kisiri ili wafiche aibu zinazoambatana na ndoa za mapema kwa familia. Bw. Waiti alisema kuwa kuna haja ya kuanzisha kampeini ya haraka kuhamasisha wazazi na viongozi kuhusu sheria zinazomtunza mtoto huku akisema kuwa kutekeleza sheria kiholela hakutaweza kuleta mafanikio bora. “Haki za watoto chini ya kipengele cha sheria za watoto, kipengele cha dhuluma za kimapenzi na katiba ni sheria ambazo zipo lakini zikifuatiliwa bila kuwaelimisha wahusika huenda zikawaathiri watoto hao hao ambao zilitungwa kuwalinda,” akasema. Alitoa mfano mathlani kama mzazi atapelekwa korokoroni, watoto hawatakuwa na mtu wa kuwalea na kusababisha kero.
Documentos relacionados
Brazil: Je, Milango ya Benki Hubaini vyuma au Rangi za Watu?
tofauti kwa kila tawi au kila mlango unaozunguka… hatuna uwezo wa kudhibiti ‘ngazi ya ufungaji’ wa kila mlango ambayo huwa kati ya ngazi ya 4 mpaka 7 (huu ni wajibu wa meneja), na hii ndiyo sababu ...
Leia mais1 Utangulizi Kitabu cha Ayubu kimepewa jina la aliye mhusika mkuu
hatia naye alikuwa mkamilifu, alimcha Mungu na kuepuka ubaya. 2Alikuwa na wana saba na binti watatu, 3naye alikuwa na kondoo 7,000, ngamia 3,000, jozi 500 za maksai, punda 500, tena alikuwa na idad...
Leia maisMathayo-Na-Petrillo-Na-Mwakabanje
Hili linaweza kufafanuliwa kwa jinsi vitenzi vya aina moja vilivyotumika katika baadhi ya misemo.
Leia mais